Posts

Showing posts from May, 2023

Nguu za Jadi - Sifa na umuhimu wa wahusika

  SIFA NA UMUHIMU WA WAHUSIKA. 1. MANGWASHA Huyu ndiye mhusika mkuu katika riwaya. Ni mkewe Mrima na mhazili wa Chifu Mshabaha. Hulka za Mangwasha: Mvumilivu Mangwasha anavumilia matatizo mengi ndani ya ndoa yake yanayotokana na ulevi wa mumewe. Hata baada ya kukimbiwa na Mrima, anavumilia mateso mengi ya ukosefu wa pesa za kuwatunza wanawe, kukiwemo pia kejeli za Sagilu. Mzalendo Mangwasha anaonyesha uzalendo pale anapotamani kukutana na viongozi wa Matuo ili amani iweze kudumishwa nchini. Anajali sana mustakabali wa nchi ya Matuo hasa pale anapowaona watoto na vijana wakiteseka bila matunzo mema ya wazazi wao au hata ajira. Mwenye matumaini Haonekani kufa moyo bali anaonyesha matumaini pale Chifu Mshabaha anapomdharau na kumdhalilisha akiwa kazini. Anaonyesha matumaini pale anapohangaika kutunza wanawe dhidi ya mateso aliyokuwa akipitia alipokimbiwa na Mrima. Anapochomewa nyumba yake pamoja na wenyeji wa Matango havunjiki moyo bali anakuwa na tumaini. Jasiri Mangwasha anaonyesha ujas

Nguu za jadi - Muhtasari wa Matukio Katika Riwaya

  Muhtasari wa Matukio Katika Riwaya Riwaya inapoanza, mhusika mkuu, Mangwasha, yuko na wanawe wawili, Sayore na Kajewa, katika kanisa fulani, ambapo wanajificha. Nje ya kanisa hilo, wapo watu wengine wa kabila la Waketwa waliokimbilia usalama hapo baada ya makao yao katika eneo la Matango kuchomwa. Kuna fununu kwamba jamii ya Waketwa inafurushwa kutoka makwao kwa sababu kuna watu fulani wanaotaka ardhi ya Matango kwa nguvu. Mtemi Lesulia, kiongozi wa nchi, anachukia kabila la Waketwa kwani yeye anatoka katika kabila la Wakule. Waketwa na Wakule wana uhasama wa tangu jadi. Inabainika kuwa Lonare, ambaye ni kiongozi wa Waketwa, ana umaarufu mkubwa nchini. Katika uchaguzi mkuu uliopita,angeshinda lakini alitekwa nyara kabla ya uchaguzi na kwa sababu hiyo, Mtemi Lesulia aliishia kuchaguliwa bila kupingwa. Mangwasha ni mwanamke mwenye bidii, na anafanya kazi ya uhasibu katika afisi ya Chifu Mshabaha. Chifu huyu ni rafiki mkubwa wa Mtemi Lesulia, naye pia anawachukia Waketwa. Hivyo, anapang