Nguu za Jadi - Dhamira ya mwandishi
Dhamira ya mwandishi Dhamira ni shabaha,nia, kusudi, au lengo kuu la kazi ya fasihi. Aidha inaweza kuwa ni shinikizo kuu liliopelekea utunzi au uwasilishaji wa kazi za kisanaa fasihi ikiwemo. Katika riwaya ya Nguu za Jadi, mwandishi anamulika masuala yafuatayo: a) Anakemea ukabila uliosakini katika jamii na unaodumaza maendeleo ya nchi. b) Anatuonyesha jinsi ufisadi unavyoweza kubomoa asasi za kijamii na kufukarisha wananchi kiasi cha kutoweza kujiendeleza kimaisha. c) Anatuonyesha jinsi ufisadi unavyoweza kusambaratisha uchumi wa nchi hasa pale unapochangiwa na uongozi mbaya kama vile ilivyotukia katika riwaya ya Nguu za Jadi. MAUDHUI KATIKA RIWAYA YA NGUU ZA JADI Ukabila/Unasaba Ukabila ni hali ya kupendelea mtu, watu au Jamii fulani kutokana na misingi ya jamii/kabila alimotoka. Upendeleo huu huweza kuhusisha mambo mengi kama vile ajira, elimu, makazi, vyeo, na kadhalika. Katika riwaya hii, ukabila